Savvy FM
Savvy FM
28 July 2026, 12:18 am

Watoto mapacha watano waliozaliwa njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru),waliozaliwa usiku wa kuamkia Julai 26,2026 wamefariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu.
Na Mariam Mallya
Watoto hao walizaliwa wakiwa na umri wa miezi sita pekee baada ya mama yao kuanza kupata uchungu wa kujifungua kabla ya wakati katika hospitali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Caren Lema ambaye ndio mama wa watoto hao amesema alijifungua watoto wanne wakiwa hai, lakini walifariki muda mfupi baadaye, huku mtoto wa tano akizaliwa tayari akiwa amefariki.
Naye baba wa watoto hao Robert Frenk amesema familia yake imepata pigo kubwa kutokana na vifo vya watoto waje nakueleza kuwa alikuwa tayari amejianda kuwapokea na kuwalea watoto wake, matumaini hayo yamekatishwa ghafla na vifo vya watoto hao.
Kwa upande wa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru amesema vifo hivyo vilitokana na mama huyo kuanza kupata uchungu kabla ya wakati kutokana na kutanuka kwa mlango wa kizazi.