Savvy FM

Youlead Summit 2026 tumaini jipya kwa vijana Afrika

31 May 2026, 5:29 pm

Waziri wa maendeleo na vijana Joel Nanauka akizungumza na waandishi wa habari.

Zaidi ya vijana 300 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wameshiriki katika Kongamano la YouLead Summit 2026 linalofanyika katika kituo cha MS TCDC kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei 2026.

Na Gasper Sambweti

Kongamano hilo limewakutanisha vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kwa lengo la kujadili na kuamua masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya bara hilo, ikiwemo amani, haki, uvumilivu pamoja na ushiriki wa vijana katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, aliwakumbusha vijana kuwa wana jukumu kubwa la kulinda, kuutetea na kuhakikisha amani pamoja na utulivu vinaendelea kuwepo katika nchi za Afrika.

Sauti ya waziri wa maendeleo na vijana Joel Nanauka

Aidha, vijana walioshiriki katika kongamano hilo wameeleza shauku yao kubwa ya kuleta mapinduzi ya maendeleo kupitia njia mbalimbali za kiuchumi. Pia walimpongeza Waziri Joel Athur Nanauka kwa hotuba yake iliyolenga kuwajenga vijana, kuwainua kiuchumi pamoja na kuwahamasisha kuendelea kutunza mazingira yao.

Sauti ya baadhi ya vijana walioshiriki kingamano