Savvy FM

Jackson afariki dunia kwa kuchomwa kisu na ndugu yake Arusha

12 June 2026, 7:35 am

Picha kwa hisani ya mtandano

Hali ya majonzi na simanzi imetanda katika Kijiji cha Sokon II, Kata ya Sokon II, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha baada ya kijana mmoja aitwaye Jackson kufariki dunia kwa kuchomwa na kisu kufuatia ugomvi wa kifamilia.

Na Michael Nanyaro

Kwa mujibu wa mashuhuda, wa tukio hilo ugomvi huo ulianza jioni baada ya Mandela kurejea nyumbani na kukuta hakuna umeme. Inadaiwa kuwa alibishana na kaka yake mkubwa, Peter, kuhusu chanzo cha tatizo hilo. 

Wakati mabishano yakiendelea, Jackson aliingia kati kujaribu kuwasuluhisha ndugu zake. Hata hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya na mmoja wa ndugu aliyetambulika kwa jina moja la Mandela anadaiwa kumchoma Jackson kwa kisu na kusababisha majeraha makubwa yaliyopelekea kifo chake. 

Sauti ya Mashuhuda wa tukio

Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sokoni II Ndugu Johanes amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema tayari jeshi la polisi linashuhulikia tuko hilo nakuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni II

Tuklkio hilo limewaacha wanafamilia na wakazi wa eneo hilo katika huzuni kubwa huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo