Savvy FM
Savvy FM
29 July 2026, 9:36 pm

Katibu na Itikadi na uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arumeru, Nicholas Sawa, ameibua hoja kuhusu ubovu wa barabara pamoja na hali ya mitambo ya ujenzi inayotumiwa na halmashauri ya wlaya ya Arusha (Arusha DC), akisema changamoto hizo zimeendelea kuwa kikwazo kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.
Na Mariam Mallya
Nicholas Sawa amesema wananchi wa maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hiyo wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara kwa muda mrefu, hali inayosababisha ugumu wa usafiri na usafirishaji wa mazao, bidhaa pamoja na huduma muhimu.
Ameeleza kuwa baadhi ya mitambo ya kutengeneza barabara inayomilikiwa na halmashauri imeharibika kwa muda mrefu, huku mingine ikidaiwa kutotumika ipasavyo, jambo ambalo limechangia kuchelewesha matengenezo ya miundombinu hiyo.
Katibu Mwenezi amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi yanayodai kuwa baadhi ya mitambo hiyo imekuwa ikikodishwa badala ya kutumika kuhudumia wananchi.