Savvy FM
Savvy FM
26 September 2026, 11:52 pm

Vijana wanne wamenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kujaribu kufanya wizi wa studio katika eneo la Soko Barazani, Kijiji cha Naurei, Wilaya ya Meru, Mkoa wa Arusha.
Na Gasper Sambweti
Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya kuanza kwa msako wa kuwatafuta na kuwakamata vijana hao, ambao inadaiwa walinaswa na kamera za CCTV wakati wakijaribu kufanya jaribio hilo la wizi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mashuda vijana hao walijaribu kufanya wizi majira ya saa sita za usiku katika eneo hilo.Baada ya msako huo kuanza, wananchi waliwakamata watuhumiwa hao nakuanza kuwaadhibu kabla ya Jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kuwachukua watuhumiwa hao.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Soko Barazani, Richard Keche amesema watuhumiwa hao waliokamatwa wamekuwa wakijihusisha na matukio mengine tofauti ya wizi katika mitaa hiyo jambo ambalo amewataka vijana kuacha kujiingiza katika makundi ya ovyo ambayo yanaweza kuweka maisha yao hatarini.