Savvy FM

Mkataba wa barabara ya Giriki-Mathias wasainiwa

29 October 2026, 8:52 pm

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Nicodemus Tambo akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa barabara. Picha na Gasper Sambweti

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Nicodemus Tambo, hivi karibuni ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara ya Giriki hadi Mathias Manga kwa kiwango cha zege, hatua inayolenga kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji katika eneo hilo.

Na Gasper Sambweti

Wakati wa hafla hiyo DC Tambo aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya barabara hiyo na kutumia fursa zitakazotokana na uwepo wake kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali za biashara.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Nicodemus Tambo.

Kwa upande wake,Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian, amewataka wananchi wa Kata ya Sakina kutunza barabara hiyo pamoja na kuzingatia utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwanufaisha wananchi.

Sauti ya meya wa Jiji la Arusha, Maximilian

Naye Diwani wa Kata ya Sakina,Hilary Daniel Mollel, amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini ambaye pia ni Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, kwa kumuunga mkono katika hatua za awali za mchakato wa upatikanaji wa barabara hiyo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Sakina,Hilary Daniel Mollel.

Ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuwa na umuhimu katika kurahisisha usafiri na usafirishaji, kukuza shughuli za kiuchumi na kuboresha huduma kwa wananchi wa Kata ya Sakina na maeneo yanayozunguka.