Savvy FM

Waziri Kadogosa aitaka TBA kujitegemea

23 November 2026, 11:25 pm

Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Mariam Mallya

Waziri Kadogosa amemuagiza Mkurugenzi wa TBA kuhakikisha wapangaji wanaodaiwa kodi za nyumba za Serikali na kushindwa kulipa wanafungiwa mifumo ya kuingia katika nyumba hizo kwa kutumia teknolojia ya Smart Lock, hadi watakapokamilisha malipo ya madeni yao.

Na Renalda Massawe

Ametoa maagizo hayo leo Novemba 23, 2026, jijini Arusha, wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa jengo la makazi la TBA lililopo eneo la Kaloleni, ambapo amesisitiza umuhimu wa wakala huyo kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo na majengo inayoyamiliki ili kuongeza mapato na kupunguza utegemezi wa Serikali.

Sauti ya Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa

Waziri Kadogosa amesisitiza kuwa TBA inapaswa kuangalia upya namna ya kuendeleza miradi yake kwa kushirikiana na taasisi za kifedha, hususan benki, ili mitaji inayohitajika kupatikana kupitia uwekezaji na ubia badala ya kusubiri fedha za ruzuku kutoka Serikalini.

Akijibu maelekezo hayo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Bw. Saidi Rajabu Mndeme, amesema wamepokea maagizo ya Waziri na watafanya mapitio ya namna bora ya kuendeleza eneo hilo kwa kushirikiana na benki.

Sauti ya mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Bw. Saidi Rajab

Hatua hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa TBA kutumia rasilimali ilizonazo kuzalisha mapato, kuongeza uwekezaji katika sekta ya majengo na kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali, huku matumizi ya teknolojia ya Smart Lock yakitarajiwa kuwa sehemu ya mikakati ya kudhibiti madeni ya kodi za nyumba za Serikali.