Savvy FM

Makonda atoa onyo kali kwa mgambo Arusha

8 October 2026, 11:04 am

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Paul Makonda akizungumza na wafanyabiasha katika soko la Kilombero Arusha.Picha na Gasper Sambweti

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Paul Makonda amewapiga marufuku mgambo jijini Arusha kuchukua bidhaa za wafanyabiashara kwani wanategemea biashara zao ndogondogo kuendesha maisha yao ya kila siku.

Na Gasper Sambweti

Akizungumza kuhusu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wadogo akiwa katika soko la Kilombero Jijiji Arusha, Mbuge Paul Makonda amesema baadhi yao wameamua kujiajiri kwa kuuza bidhaa mbalimbali kama nyanya, mchicha, pilipili, vitunguu na karotii ili kujipatia kipato na kuhudumia familia zao hivyo hawapaswi kusumbuliwa.

Amesema wapo pia wanawake wanaolea watoto peke yao baada ya kutelekezwa na wenza wao, hivyo wanategemea biashara ndogo ndogo kama chanzo cha chakujipatia kipato.

Makonda amesema malalamiko ya wafanyabiashara hao yanahusisha pia mgambo kuchukua bidhaa zao, kuwafanyia ukatili na kuwapiga, akisisitiza kuwa jambo hilo halipaswi kuendelea huku akisema viongozi wana wajibu wa kusimamia watendaji ili kuhakikisha wananchi wanapata haki na mazingira salama ya kufanya shughuli zao za kujipatia kipato.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini Paul Makonda