Savvy FM

Madereva wa mabasi Arusha walia na serikali

30 September 2026, 2:44 am

Meneja msaidizi kampuni ya Shabbyline kanda ya kaskazini, Nurudin akizungumza kuhusu mgomo wa mabasi. Picha na Gasper Sambweti

Madereva wa mabasi yaendayo mikoani jijini Arusha wameungana na madereva wengine nchini kusitisha kwa muda huduma za usafirishaji, wakieleza kutoridhishwa na mfumo wa ukataji wa alama kwenye leseni za udereva.

Na Gasper Sambweti

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa Septemba 2026, mfumo huo unahusisha alama 15 kwenye leseni, ambazo hupunguzwa dereva anapobainika kufanya makosa mbalimbali ya barabarani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva wa mabasi wamesema hali hiyo imekuwa ikiwaathiri nakuiomba mamlaka kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo ili waweze kuendelea na kazi zao bila vikwazo vyovyote.

Sauti za madereva wa mabasi ya mkoani

Nao baadhi ya wananchi wamesema hatua hiyo imeathiri shughuli za usafirishaji pamoja na biashara zinazofanyika katika stendi huku baadhi ya wasafiri wakieleza namna ambavyo wamepata usumbufu na hasara kwa kushindwa kusafiri kutokana na kutopata taarifa za mgomo huo mapema.

Sauti za wananchi na wafanyabiashara

Hatahivyo kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Awadh Juma Haji, ametolea ufafanuzi nakusema kuwa Jeshi la Polisi litawachukulia hatua kali wanaozuia mabasi na malori kutembea barabarani .

Sauti ya CP Awadh Juma Haji