Savvy FM
Savvy FM
24 November 2026, 6:42 pm

Jukwaa maalumu la wadau wa mfumo wa haki Jinai nchini limekutana jijini Arusha lengo kuu likiwa ni kubadilishana uzoefu katika kuimarisha upelelezi na uendendeshaji wa mashauri kwa wadau wa mfumo wa haki jinai.
Na Mariam Mallya
Serikali kupitia wizara ya katiba na sheria imeendelea kuwajengea uwezo wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika kutambua na kukusanya vielelezo eneo la tukio kwa kuzingatia sheria.
Akizungumza na wataalamu hao Naibu Katibu mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Balozi Baraka Luvanda amesema udhibiti uhalifu wa kimtandao ni miongoni mwa mambo ya msingi kwa wadau hao kubadilishana uzoefu bila kuathiri faragha za wengine kwa mujibu wa sheria na miongozo,
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki katika Wizara ya katiba na sheria, Jane Lymo alieleza namna ambavyo mwananchi naenda kunufaika kwa kuzingatia matizamo chanya ya Teknolojia na sayansi.