Savvy FM
Savvy FM
1 October 2026, 12:11 am

Hali ya usafiri wa mabasi katika mkoa wa Arusha imerejea kuwa ya kawaida baada ya mgomo wa madereva ulioibuka toka jana , isipokuwa kwa mabasi yanayofanya safari kuelekea Dar es Salaam.
Na Gasper Sambweti
Akizungumza na Savvy Fm, Mwenyekiti wa Mawakala wa Usafirishaji Jiji la Arusha, James Leonard, amezishukuru mamlaka zinazohusika kwa hatua zilizochukuliwa kurejesha hali ya usafiri.
Mwenyekiti huyo amesema kurejea kwa usafiri utafanya mambo kuendelea kama kawaida na kuwataka wasafiri kuendelea kukata tiketi kwa ajili yakupata huduma kama kawaida.
Leonard ametoa wito kwa wasafirishaji kuendelea na shughuli zao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa, akisisitiza umuhimu wa kufanya shughuli za usafirishaji kwa utaratibu na kwa kuzingatia usalama wa abiria.