Savvy FM
Savvy FM
1 September 2026, 2:25 pm

Wananchi Katika Mtaa wa RC na Mbeshere kata ya Oloirien jijini Arusha waililia serikali kutokana vitendo vya wizi wa miundombinu ya maji, ikiwemo mita za maji, get valve pamoja na koki za mabomba unaoendelea katika maeneo yao.
Na Gasper Sambweti
Wakieleza kilio chao wananchi hao wamesema kuwa wizi huo umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa huduma ya maji, huku ukiwaathiri pia kiuchumi kutokana na gharama wanazolazimika kutumia kurejesha miundombinu hiyo.
Wamesema vitendo hivyo vinawarudisha nyuma katika jitihada zao za kupata huduma ya maji kwa uhakika na kuwataka wahusika kuacha kuhujumu miundombinu inayolenga kuwahudumia wananchi.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa RC Benedict Kawishe wameiomba mamlaka husika kuingilia kati sakata hilo na kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na wizi na uharibifu wa miundombinu ya maji.