Savvy FM
Savvy FM
27 June 2026, 1:18 am

Jamii imetakiwa kuendelea kuungana katika mapambano dhidi ya matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya, huku elimu ikitajwa kuwa silaha muhimu katika kuokoa maisha ya vijana.
Na Mariam Mallya
Kauli hiyo imetolewa katika na Afisa Kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa ya kulevya kanda ya kaskazini Abdulatif Said wakati akizungumza na Savvy Fm ambapo amesema maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya hufanyika june 26, 2026 na kwa kanda ya kaskazini wameamua kuutumia mwezi wote kutoa elimu kwa jamii kuhusu dawa za kulevya.
Aidha amesema vijana wamekuwa waathirika wakubwa wa dawa ya kulevya kutokana na kukukosa elimu pamoja na kufuata mkumbo wakiwa na umri mdogo na kuwataka wazazi kuwalea watoto katika maadili na kuwachunga nakutokuwapa uhuru uliopitiliza.