Savvy FM

Pombe yatajwa chanzo cha ukatili, vifo kwenye jamii

27 June 2026, 10:51 am

Meneja Mradi kutoka Blue Cross Society of Tanzania, Bi. Gloria Vicent.

Takribani kifo kimoja kati ya vifo vitatu nchini kimehusishwa na matumizi ya pombe, huku wataalamu wakisisitiza haja ya serikali na taasisi husika kutoa takwimu sahihi kuhusu athari za pombe na dawa za kulevya ili kulinda jamii dhidi ya madhara yake.

Na Peter Spirit

Hayo yameelezwa na Meneja Mradi kutoka Blue Cross Society of Tanzania, Bi. Gloria Vicent, shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kampeni za elimu ya jamii kuhusu madhara ya pombe na dawa za kulevya, wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Arusha, ambapo amesisitiza kuwa zaidi ya asilimia 40 hadi 60 ya vifo vinatajwa kuhusishwa na matumizi ya pombe.

Sauti ya Meneja Mradi kutoka Blue Cross Society of Tanzania, Bi. Gloria Vicent.

Naye mwandishi mkongwe Asraji Mvungi, amesema elimu hiyo inapaswa kufikia jamii kwa upana zaidi ili kusaidia kupunguza ukatili wa kijinsia unaochochewa na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

Sauti ya mwandishi Asraji Mvungi