Savvy FM

Wavunja sheria waonywa Arusha

14 September 2026, 11:52 am

Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iraqwe akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Picha na Gasper Sambweti

Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iraqwe amewataka viongozi katika halmashauri ya Arusha kufanya kazi kwa kufuata sheria na kuepuka kusababisha sintofahamu katika jiji hilo.

Na Gasper Sambweti

Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa ajili ya kuweka taa za barabarani  ili kuhimarisha miundombinu ya usalama ya jiji hilo.

Meya Iraqwe ameeleza kuwa watatoa kipaumbele kuweka taa sehemu zenye watu wengi kama katika masoko na stendi za mabasi

Sauti ya Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iraqwe

Aidha stahiki meya amewataka wamachinga pamoja na madereva kufuata sheria na taratibu zilizowekwa nakusema jiji la Arusha haliendeshwi kwa mazoea bali linaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria hivyo hawata mvumilia mtu yoyote atakaye vunja sheria.

Sauti ya Meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iraqwe