Savvy FM

Maonyesho ya Hortilogistica Afrika 2026 yafunguliwa Arusha

9 November 2026, 10:15 pm

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Hortilogistica yaliofanyika jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amefungua rasmi maonyesho ya kimataifa ya mbogamboga,Viungo, matunda na maua Maarufu kama HortiLogistica Africa 2026, ambapo serikali imesisitiza mamlaka na taasisi za kilimo kuendelea kufungua masoko ya kimkakati kwa kuzingatia ubora wa bidhaa na fursa kwa wakulima.

Na Mariam Mallya

Akifungua jukwaa hilo la kimataifa la wadau wa sekta ya kilimo cha mazao ya Horticulture na biasahara Jijiji Arusha baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho, kwa waoneshaji zaidi ya 150 Barani Afrika, Mhe.Ndejembi ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),Wizara ya Kilimo, kwa kushirikiana na wadau waliopo katika mnyororo wa thamani kuongeza juhudi za kufungua masoko ya kimkakati Afrika na duniani kwa ujumla kwa kuzingatia viwango vya mahitaji ya soko la dunia.

Sauti ya Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi

Naye Waziri wa Kilimo, Daniel Chongollo, amesema mazao ya horticulture yamekuwa fursa ya kuwafungulia dunia wakulima na vijana walio wekeza katika kilimo hicho.

Sauti ya waziri wa Kilimo, Daniel Chongollo