Watu wenye ulemavu pemba walia na kitengo cha elimu ya afya
12 August 2022, 8:40 am
PEMBA
Ufikiwaji mdogo wa watu wenye ulemavu katika utoaji wa elimu ya chanjo ya uviko 19 ni changamoto moja wapo inayopelekea ushiriki mdogo kwa kundi hilo.
wakizungumza na mkoani fm mariam khamis hamadi na nasra hakim hassani wenye ulemavu wa viungo wamesema tangu kuanza kwa ugonjwa huo hawakuzingatiwa ipasavyo katika kupewa elimu hali inayopelekea kukosekana kwa ushiriki katika zoezi la kuchanja chanjo ya uviko 19.
mkurungenzi mtendaji kutoka jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar Shahib Abdallah Muhammed ameshauri idara husika kwani ipo haja sasa kwa kundi hilo kupewa kipaumbele ili kuhamasika na kujitokeza kuchanja.
asma khamis Mratibu T-MARC, zanzibar amekiri kuwepokwa changamoto hiyo na taasisi yao kwa kushirikiana na kitengo cha elimu ya afya imeamua kutoa elimu kwa kundi la watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwafikia ipasavyo.
Dr Omar Makame afisa elimu wilaya ya mkoani amesema wizara kupitia kitengo cha elimu ya afya inayo mikakati imara katika kuwafika waatu wenyewe ulemavu kwani imeshaanza kupita katika mitaa na kutoa elimu ya kuwataka kukubali chanjo ya uviko 19 ili kujikinga na ugongwa huo.
Jumla ya watu 23 wa wenye ulemavu wamechanja baada ya kupata elumu ya umuhimu wa chanjo ikiwa ni sehemu kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.