Uchumi wa buluu kuwainua vijana Pemba
8 September 2023, 9:40 am
Vijana wanatakiwa wasisubiri ajira serikalini bali wajishugulishe kwenye shuguli mbali mbali zikiwemo fursa za uchumi buluu kwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiariamali ili waweze kujiengezea kipato
Vijana wameonywa kuepuka kukaa katika vigenge viovu ,na badala yake wajiunge na vikundi vya ushirika, ili waweze kujipatia kipato cha halali.
Ushauri huo umetolewa na katibu wa kikundi cha ushirika mapambano coperetive kinacho jishuhulisha na ufugaji wa Samaki, kaa, kamba na mboga mboga Bishara Muhammed Musa mbele ya wanakikundi hao, mara baada ya kutembelewa na wajumbe kutoka wizara ya uchumi wa Buluu na shirika la International Union for conservation of Nature [IUCN] kutoka Tanzania bara huko Sizini wilaya ya Miheweni Mkoa wa Kaskazi Pemba.
Ameeleza wakati umefika kwa vijana kuwamka na kujiajiri wenyewe, na sio kukaa tu vigengeni na kusubiri ajira Serikalini.
Aidha alieleza kuwa sera ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya uchumi wa buluu unaelekeza zaidi kwenye bahari, hivvyo aliwasisitiza viajana hao kukiendeleza kikundi chao kwa juhudi zote, jambo ambalo litawawezesha kupata ursa mbali mbali za kimaendeleo.
Mapema mwanakikundi Khadija Ali Juma alieleza kuwa ameamua kujiunga kwenye kikundi cha ujasiriamali, ili aweze kujipatia kipato kitakacho msaidia katika familia yake.
Aidha amesema mafanikio hayaji tu kama ndoto, hivyo ni vyema kuwa wavumilivu kupitia changamoto zinazowatokezea ili waweze kukiikisha mbele kikundi chao.
Mwenyye kiti wa kikundi hicho Khalfan Hamad Khalfan alieleza kuwa matarajio yao ni kuhakikisha wamekuwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya baharini.
Hivyo aliomba wizara ya uchumi wa buluu kujitokeza na kuwaunga mkono vikundi ambavyo vimewekeza juhudi zao kwenye maeneo ya bahari, ili waweze kunufaika na fursa zilizomo, ndani ya sera ya uchumi wa buluu.
Nae afisa kutoka wizaa ya uchumi wa buluu Pemba Mohd Ali pamoja na wajumbe kutoka shirika la International Union for conservation of Nature [IUCN] ni kuangalia maendeleo yao, na kuelewa changamoto zinazo wakabili wanakikundi hao na kuweza kutatuliwa.
Kkikundi hicho ambacho kinawanachama 17 wanaume 8, na wanawake 9, ambacho kilianza rasmi mwaka 2013.