Kilio kwa wananchi wa Mjini Kiuyu kutotumika jengo lao la kituo cha Afya
8 September 2023, 9:01 am
Wananchi wa Mjini Kuyu Wilaya ya Wete wakililia miaka 12 tangu kujengwa kituo cha Afya katika kijiji chao kwa lengo la kusaidia kwa mama wajawazito kupata huduma kwa wakati ila bado seriakali hawajakitumia kituo hicho kama wanavyohitaji wananchi hao.
Na Fatma Hamad.
Wananchi wanaoishi kijiji cha Mjini Kuyu Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wavunja ukimya na kutoa kilio chao kutokana baada ya kuwekeza nguvu na pesa zao kwa ajili ya kujenga kituo cha afya, lakini kimeshindwa kutumika na kutoa huduma kwa sababu ya kukosekana kwa wahudumu wa Afya .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Mwananchi khamis Omar ameeleza kuwa walifanya mchango nyumba hadi nyumba wa vifaa vya ujenzi pamoja na kushiriki katika ujenzi na kujenga kituo cha afya, na Serikali ikawasaidia katika kuwezeka kituo hicho.
Hata hivyo, tokea mwaka 2011 mpaka sasa kituo hicho hakitumiki na kimekuwa gofu.
Amesema huu ni mwaka wa 12 tokea kujengwa kwa kituo hicho, ambapo kilifunguliwa na mbio za mwenge kwa shangwe na nderemo, ili kuondosha shida za wananchi wa kijiji hicho.
Ameeleza baada ya kuona wanapata tabu kwa kufuata huduma za afya masafa marefu, ndipo wakamua wao wenyewe kujitolea kujenga ili waondokana na kadhya hiyo, lakini bado wanaendelea tu kuteseka.
Mapema mwanachi Raya Hassan Amesema kukosekana kwa kituo cha afya karibu na makaazi yao wanapata shida hususan wanapopata mgonjwa wakati wa usiku.
Ameeleza wanachukua masafa kilo mita nne kufuata huduma ya afya, ambapo wanalazimika kupita sehemu za vichaka na mabonde.
Aidha ameeleza kuwa kukosekana kwa kituo cha afya kunachangia kwa kiasi kikubwa wa mama wajawazito kujifungulia majumbani.
Amesema kuwa uzazi wa sikuhizi ni mashaka, hivyo ni vyema kituo kiweze kutoa huduma ili kulinda usalama wa mama na mtoto.
Diwani wa wadi hiyo Bi Nasra amesema yeye pamoja na sheha tayari wameshafuatilia kila sehemu ili kuona kituo hicho kinatoa huduma, lakini imeshindikana.
Afisa mdhamini wizara ya Jinsia na maendeleo ya jamii Khamis Bilal Ali alifahamisha kuwa wanajenga Hospitali katika eneo la kiuyu minungwini ambayo itawanufaisha wananchi wa Minungwini pamoja na wa mjini kuyu.
Amesema kuwa jingo hilo walilolijenga watalitumia kukiwa na kesi maalumu kama vile mripuko wa maradhi pamoja na kipindi cha utoaji wa chanjo za watoto.