Mkoani FM

Wananchi Wilaya ya mkoani wahimizwa kuwa na Ushirikiano wa kutosha 

5 August 2025, 8:36 am

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki (Picha Said Omar)

Wananchi wa kiwani wametakiwa kutoa mashirikiano katika kupunguza uhalifu katika eneo pia wananchi hao wameliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua wahalifu wanapopekwa kituoni

KHATIB JUMA NAHODA

WANANCHI wa Shehia ya Kiwani Wilaya ya Mkoani Pemba wamelitaka Jeshi la Polisi Wilayani humo kushirikiana na kwa karibu na Polisi jamii ili kudhibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo wizi wa mifugo katika Shehia yao.

Wamesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiwani sokoni ulikuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi hao.

Wameeleza kuwa walieleza kuwa  wizi wa mazao na mifugo umekithiri katika maeneo yao  hali ambayo  inaleta hofu na kutishia usalama wao na juhudi za kupambana na umaskini.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya mkoani Miza Hassan Faki amesema vitendo vya wizi wa mazao na mifugo, ni tatizo linalorudisha nyuma juhudi za wakulima na wafugani na kusababisha migogoro mikubwa katika jamii.

Amewataka wananchi kutowa ushirikiano wao katika kupambana na vitendo vya wizi wa mazao kwa kushirikiana na Polisi jamii kwani watendaji wa mambo hayo wanatoka ndani ya jamii zao.

Akizungumzia kuhusu uvunjaji wa maadili DC Miza amekemea vikali mavazi yasiyozingatia maadili, hasa kwa vijana, na kusisitiza kuwa jamii inapaswa kuenzi mila, desturi na utamaduni na kuwataka wazazi wakiume kusimama katika nafasi yao ya msingi kama nguzo ya familia na sio kuwaachia kina mama peke yao.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Miza Hassan Faki

Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani, Utulivu na mshikamano hasa katika kipindi hichi Taifa linapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu wa 2025 kwani bila ya amani hakuna linaloweza kufanyika.

Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu OCD wilaya ya Mkoani Bakar Juma Kombo  amesema lengo la kuanzisha na kuimarisha Polisi shirikishi ni kujenga mahusiano ya karibu kati ya Polisi na wananchi kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti uhalifu kwa njia ya ushirikiano.

“Ili Polisi jamii iweze kufanya kazi zake vizuri ni lazima kuwepo na mashirikiano makubwa baina yao na wananchi wakiwemo wazazi”, ameeeleza.

Kaimu OCD wilaya ya Mkoani Bakar Juma Kombo (Picha na Said Omar)

Nao Wananchi waliohudhuria wamempongeza kiongozi huyo kwa kugusa masuala yanayowakera moja kwa moja, huku wakiahidi kushirikiana naye katika kujenga jamii yenye maadili, amani na maendeleo.