Kamati za mitihani Zanzibar zatakiwa kuzingatia maadili
27 October 2023, 6:14 pm
Kufuatia kufanyika mitihani ya taifa ya hivi karibuni Zanzibar, kamati maalum za usimamizi zimetakiwa kuwa waaminifu kwenye usimamizi wao na kuhakikisha wanafanya kazi inavyotakiwa kwa kufuatia miongozo yao.
Na Amina Masoud.
Kamati za za mitihani za mikoa na wilaya zimetakiwa kuhakikisha kuzingatia kanuni na miongozo ya uendeshaji wa mitihani ya taifa iliyotolewa na baraza la mitihani la Zanzibar.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amili Zanzibar Leila Muhamed Mussa wakati wa mkutano wa waandishi wa habari ulifanyika katika ukumbi wa wizara hiyo chakechake Pemba, amesema ni muhimu kwa kamati hizo kuhakikisha zinazingatia usalama wa vituo vya mtihani na kuzia udanganyifu.
Amesema wakati wa mitihani kunatokea mambo mengi ya udanganyifu jambo ambalo hupelekea kwa baadhi ya wanafunzi kufutiwa matokea hivyo ni vyema kuwa makini na kuondoa udanganyifu kwani wizara imejiandaa vizuri kukabiliana na changamoto hiyo.
Akigusia kuhusu kufanya mitihani kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Lela amesema wizara imejipanga na kuwaandalia mitihani kulingana na mahitaji yao, ambapo kwa wenye uoni hafifu wameandaliwa mitihani kwa hati zilizokuzwa.
Amewataka wakuu wa vituo na wasimamizi wafanye kazi zao kwa kuzingatia miongozi ya baraza la mitihani Zanzibar na kuhakikisha kuwa wanatoa haki kwa watahiniwa wenye mahitaji maalum miongoni mwa kuongeza muda wa nusu saa kwa kila saa moja ya mtihani na wale wa uoni hafifu wanapewa mitihani inayowahusu.
Jumla ya watahaniwa 58,485 kwa darasa la nne na 44,684 kwa darasa la saba na 24,382 kwa kidato cha pili na vituo vya mitihani kwa darsa la saba ni 545, darasa la nne 451 na kidato cha pili 313 Mitihani inayotarajiwa kuanza 30/10 hadi 02/11/ 2023, na darasa la nne 6/11 hadi 08/11/2023na kwa kidato cha pili yataaanza 04/12 hadi 12/12/2023. Huku watahaniwa wenye mahitaji maalum ni 655, kati ya hao darasa la nne 289, darasalasaba242 nakidato chapili ni 1124 wanaotarajiwakufanyamtihani mwaka huu.