Utafiti maskulini wagundua lishe za wanafunzi ziko chini masheha wapewa kazi kwa jamii Pemba
26 October 2023, 10:21 am
Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar kwa kushirikiana na wizara ya afya watatoa virutubisho vya lishe kwa wanafunzi kwa lengo la kuimarisha afya zao.
Na Amina Masoud
Masheha kisiwani Pemba wametakiwa kutoa mashirikiano katika kampeni ya utoaji wa Elimu Kwa jamii juu ya umuhimu wa virutubisho lishe skulini Ili kuleta afya Bora Kwa wanafunzi.
Akizungumza na masheha wa wilaya ya Chakechake Afisa mdhamini wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Pemba Mohammed Nassor Salim amesema masheha wana nafasi kubwa katika kuifikia jamii hivyo ni vyema kutumia fursa hiyo kutoa mashirikiano ili lengo liweze kufikiwa.
Amesema wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar baada kufanya utafiti na kugundua kuwa lishe za wanafunzi ziko chini imeamua kuja na kampeni ya kutoa virutubisho skuli zote za Zanzibar Ili kuleta vijana wenye afya imara.
Akimkaribisha mgeni rasmi mratib wa lishe kutoka wizara ya Elimu Zanzibar Zulfat Kabanga amesema mashirikiano ya pamoja kati ya masheha wazazi na walimu yatapelekea kufikisha lengo lililokusudiwa na kupata taifa lenye vijana wenye afya bora.
Kwa upande wake Hafidh Saleh Afisa lishe kutoka wizara ya Elimu amesema utafiti huo umefikia wanafunzi 2559 Kuanzia umri wa miaka 5 Hadi 19 Kwa skuli 93 katika wilaya 11 za Zanzibar
Akichangia mada katika kikao hicho Abdallah Mohd Said katibu wa sheha vitongoji ameiomba wizara ya Elimu kuwashauri wanaouza vyakuli skuli kuuza vyakula vya asili ili kurejesha afya Kwa waanfinzi.
Mradi wa kutoa virutubisho kwa wanafunzi ni mradi wa miezi 10 unaofadhiliwa na UNICEF na kutekelezwa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar.