Viongozi wa dini watakiwa kufikisha elimu ya lishe Pemba
24 October 2023, 8:47 am
Kuwepo kwa upungufu wa virutubisho lishe kwa jamii wizara ya elimu na mafunz, ya amali kwa kushirikiana na wizara ya afya Zanzibar kuwasaidia wanafunzi kuwapatia virutubisho hivyo kwa lengo la kuijenga jamii yenye afya njema.
Na Amina Masoud
Viongozi wa dini kisiwani Pemba wametakiwa kutumia nafasi Yao kufikisha Elimu ya lishe Kwa jamii Ili kujikinga maradhi mbalimbali yakiwemo upungufu wa damu, maradhi ya minyoo na Lishe duni.
Wito huo umetolewa na msaidizi mkuu wa kitengo Cha Elimu ya afya Pemba Suleiman Faki Haji wakati akizungumza na viongozi wa dini na walimu wa madrsa katika mkutano wa nusu siku uliofanyika ukumbi wa skuli ya Madungu Chakechake Pemba.
Amesema viongozi wa dini wananafasi kubwa katika kuifikia jamiii kwani ni kundi ambalo linasikilizwa zaidi na Jamii hivyo ni vyema kutumia nafasi hiyo kuielimisha jamii.
Amesema utafiti uliofanywa na wizara ya elimu na mafunzo ya amali umeonesha bado Kuna uhitaji wa upatikanaji wa virutubisho lishe Kwa jamii ikiwemo wanafunzi.
Akifungua mkutano huo mratibu wa ofisi ya mufti Pemba sheikh Said Ahmad Mohammed amesema lishe ni muhimu kwani hujenga afya nzuri na hata dini inahimiza umuhimu wa kuwa na afya njema kwani huupa mwili nguvu ya kufanya kazi vizuri ikiwemo ufanisi katika ibada.
Nae mratib wa lishe Wilaya ya chakechake Harusi Massoud Ali amesema wameamua kutoa virutubisho hivyo Kwa skuli zote za Zanzibar kuanzia form one Hadi form 6 kwani kundi Hilo ndio lililosahaulika katika kupata virutubisho.
Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo wamesema wataifanyia kazi Elimu hiyo na kuifikisha sehemu husika Ili lengo liweze kufikiwa na nchi kuwa na taifa lenye watu wenye afya nzuri.
Mkutano huo ulioandaliwa na wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar kwa kushirikiana na wizara ya afya wenye lengo la kutoa Elimu ya umuhimu virutubisho lishe Kwa wanafunzi wote kuanzia form one Hadi form 6 chini ya ufadhili wa UNICEF na kutekelezwa wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar.