Kwa mara ya kwanza ndege yenye kubeba abiria 72 kuanza safari Pemba
8 October 2023, 10:26 pm
Kuwepo kwa changamoto ya usafiri wa anga kisiwani Pemba kumepelekea kuengezeka kwa kampuni nyengine ya usafirishaji abiria kwa njia ya anga.
Na Fatma Rashid.
Wazir wa ujenzi mawasoliano na uchukuzi Dr Khalid Salim Mohd amesema Ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba wenye ukubwa wa kilimita 2.5 unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ameyasema katika uzinduzi wa ndege mpya aina ya fligtlink yenye uwezo wa kubeba abiria 72 uliofanyika katika uwanja wa ndege Pemba amesema Serikali ya awamu ya nane Ina lengo la kuimariaha usafiri katika nyanja za nchi kavu baharini na katika anga hivyo kukamilisha Kwa ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba kutaimarisha zaidi.
Ameeelza kuwa kutokana na baadhi ya mashirika ya ndege kusitisha safari zao Pemba visiwa vya Zanzibar vilikuwa vinakabiliwa na changamoto ya usafiri wa anga ambayo ilisababisha baadhi ya abiria kukosa hudumu hiyo hivyo kiwepo Kwa ndege hiyo kutapungiza changamoto ya usafiri wa anga .
Mkurugenzi muendeshaji wa shirika la Ndege la Fligtlink Jameel Kassam ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaruhusu kufanya usafirishaji katika visiwa vya zanzibar na amesema kuwa shirika Hilo litatoa huduma kila siku katika nyakati tofauti.
Mkuuu wa Mkoa wa Kaskakazini Pemba Salama Mbarouk Khatib kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba amessma hatua anazozichukuliwa za kujenga uwanja wandege Pemba ni hatua ya kutatua changamoto za uwanja wa ndege Pemba na zitasaidia kuengeza kuja kwa watalii wengini kisiwani hapa
Aidha amelishukuru Shirika hilo la Ndege na kusema kuwa viongozi wa Pemba watashirikana vyema kuona ndege hiyo inakuwa salama na inafanya kazi zake kama ilivopangwa.
Ghafla hiyo ya uzinduzi wa ndege mpya ya Flightlink yenye uwezo wa kubeba abiria 72 itakayofanya safari zake unguja kwenda Pemba kila siku.