Dkt. Khalidi: Tusichafue bahari kwani asilimia 50 ya oxygen inatoka huko
29 September 2023, 4:37 pm
Wananchi waache kuchafua mazingira ya bahari ili ibaki katika haiba yake na kuwalinda viumbe hai wanaopatikana ndani yake.
Na fatma Rashid.
Waziri wa Ujenzi, Mawasoliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salim Ali ameitaka jamii kuacha tabia ya kutupa taka ovyo baharini na ukataji wa mikoko Ili kulinda mazingira safi ya bahari.
KAULI hiyo ameitoa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya bahari Dunia yaliyofanyika katika viwanja vya Gombani Chake chake Pemba amesema asilimia kubwa ya watu na viumbe vya baharini wanategemea oxygen ambayo kwa asilimia 50 inatokana na bahari hivyo ni vyema kuyatunza Ili kuendeleza Haiba ya bahari iliyopo.
Pia amesema kuwa licha ya kuwepo kwa bahari lakini bado kuna baadhi ya watu hawatambui umuhimu wa uwepo wa bahari, hivyo amewataka wananchi kuchukua hatua za makusudi kulinda na kuhifazi mazingira ya baharini.
Kwa upande wake Mkurugenzi i wa mamlaka ya usafiri majini ZMA Shekha Ahmed Mohd amesema wananchi kupitia wizara ya Uchumi wa buluu wamejikita katika shuhuli mbali mbali zikiwemo kilimo cha mwani , uvuvi ,utalii ,ufugaji wa majongoo utafutaji wa mafuta na shuhuli nyengine za kujipatia ziski ,hivyo amewataka wananchi kutunza mazingira na kufuata sheria ili kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba salama Mbarouk Khatib ameishukuru serekali ya Tanzania bara SMT kwa kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ katika kufanikisha jambo hili .
Aidha Mkurugeni wa Usalama wa Mazingira ,Wizara ya Uchukuzi Tanzania Stella Joshua Katondo amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuibua uelewa kwa watu juu ya utunzaji wa mazingira ya bahari pamoja na fursa zinazopatikana kwenye bahari.
Maadhimishi ya siku ya bahari duniani hifanyika Kila September 28 ya Kila mwaka na mwaka huu yamefanyoka ktk viwanja vya gombani chake chake Pemba na kauli mbiu ni Miaka 50 ya marpol uwajibikaji wetu unaendelea.