Vipindi vya elimu Redioni vitaengeza ufaulu Sekondari.
14 September 2023, 3:58 pm
Vipindi vya elimu vya redio zinasaidia kuengeza ufauli kwa wanafunzi hasa wa sekondari ni vyema wazazi na walimu kushirikiana kwa pamoja kuwahimiza watoto wao kufuatilia vipindi hivyo kwa lengo la kuengeza ufaulu.
Na Fatma Rashid.
Meneja wa mradi wa Secondary Radio Education ( SRE) Jun sug an Baraka amewataka wazazi na walimu kuwahamasisha wanafunzi wa sekondari kujifunza kupitia vipindi vya redio kwa lengo la kukuza ufaulu wao.
Ameyasema hayo katika ghafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha elimu kupitia vipindi vya redio Pemba iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha SAMAIL Gombani Chake Chake Pemba.
Pia amesema kuwa Elimu ndio njia pekee ya kubadilisha maisha hivyo amewataka wazazi na walimu kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuwashawishi wanafunzi kujifunza kupitia redio kwani itasadia kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza Afisa Elimu Mkoa wa Kusini Pemba Mohammed Shamte kwa niaba ya Mgeni Rasmi Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu Pemba Mohammed Nassor Salim amewashukuru KOICA na good Neighbours kwa yote waliyoyafanya katika Elimu kwani ni mambo yenye tija kwa Wizara na wanafunzi.
Hata hivyo amesema kuwa Redio ndio nyenzo muhimu sana kwa kuwahamasisha wanafunzi kuweza kujifunza na kufaulu vizuri katika masomo yao hivyo wazazi na walimu wana jukumu lao kuwasimamia watoto kujifunza.
Kwa upande wake mtoa mada ya Wazazi kusimamia watoto wao kwenye elimu Ndugu,Sabrina Ali Batashi amewasisitiza wazazi kuwashawishi watoto wao kujifunza kupitia vipindi vya redio kwani watajifunza vitu vingi vitakavowasaidia kufanya vizuri katika masomo yao
Pia amesema kuwa mzazi ndie mtatuzi mkubwa wa kutatua changamoto za mtoto na kumsaidia kuleta mabadiliko
Kwa upande wa washiriki katika ghafla hiyo wamesema kuwa ni jukumu la wazazi kuwalea watoto wote katika jamii zao kama watoto wao na kusiwe na mtu na mwanawe tu kwani jamii ili iendelee ni lazima wazazi waungane kuwalea watoto wao.
Mradi huo wa miaka bmiwili unaotekelezwa na GOOD NEGHBOURS kwa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanziabar kwa ufadhili wa shirika la ushirikiano la kitaifa korea KOICA kwa lengo la kukuza ufaulu wa Wanafunzi Sekondari wa Zanzibar kwa njia ya kujifunza kupitia vipindi vya Redio.
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la mtambwe, tume ya uchaguzi Zanzibar imeamua kufanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi hiyo iliopo wazi na wadau wote wa uchaguzi wanatakiwa kushiriki kukamilisha uchaguzi huo kama ilivyokusudiwa.