Mtu mmoja ajeruhiwa na watu wasiojuilikana Pemba
8 September 2023, 12:02 pm
Mmiliki wa kambi ya uchumaji zao la karafuu anajeruhia na watu wasiojuuilikana huko kambini kwake matukio hayo yanajitokeza kila msimu wa karafuu unapofika kisiwani Pemba.
Na Mwandishi wetu.
WATU wasiofahamika Wadaiwa kuvamia kambi ya karafuu na Kumshambulia kwa vitu vyenye ncha kali mmiliki wa kambi hiyo Machano Ali Ame mkaazi wa Bumbwini Misufini wilaya ya Kaskazini B Unguja tukio lilitokea juzi majira ya saa 5 usiku huko Chumbageni wambaa wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba
Akisimulia jinsi alivyokutwa na mkasa huo Majeruhi huyo akiwa katika hospital ya Abdalla Mzee kwajili ya matibabu amesema watu hao waliomvamia katika kambi hiyo huku akiwa usingizini jambo ambalo lilipekea kutokuwafahamu watu hao waliomshambulia kwa vile alishutuka na kupiga mayowe kwajili ya kutaka msaada wa kunusuru uhai wake.
Akithibitisha kupokea Majeruhi huyo Daktari dhamana hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Rashid Saleh Hemed amesema hali ya majeruhi huyo kwa sasa inaendelea vizuri ambapo mnamo saa sita usiku alifikishwa hospitalini hapo akiwa na majeraha mbali mbali ikiwemo sehemu za kichwa pamoja na mabega.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Siprian Alaice Mushi amekiri kupokea taarifa hizo ambapo amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .