Waandishi wa habari Pemba kupewa mbinu mpya kuandika habari za udhalilishaji
26 August 2023, 8:53 am
Waandishi wa habari Kisiwani Pemba kupatiwa mafunzo maalum ya uandishi wa habari za udhalilishaji kwa lengo la kuisaidia jamii endapo watapata kadhia hiyo.
Na Khadia Ali
Waaandishi wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kufanya ufuatiliaji wa kuzielezea na kuzichakata kwa kutumia takwimu habari zinazohusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia Ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu wa Mawasiliano kutoka TAMWA – ZANZIBAR Safia Ngalapi wakati akifungua mafunzo ya siku tatu yanayohusu uandishi wa habari za udhalilishaji amesema lengo nikuwakumbusha kuendelea kuandika habari hizo ili kuisaidia jamii.
Amesema jamii inauwelewa mdogo kuhusu dhana ya udhalilishaji na ndio mana matendo hayo yanaongezrka siku hadi siku.
Amesema utafiti uliofanywa na Shirika la Elimuna Sayansi na Utamaduni UNESCO kwa kusirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzani – Zanzibar katika kipindi cha mwezi January –March kwa baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo magazeti,radio na mitandao ya kijamii Bado haijawafikia walengwa jambo ambalo linapelekea kukithiri Kwa vitendo hivyo.
Akiwasilisha mada ya majukumu ya waandishi wa habari mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Aiman Duwe amesema ni kuchunguza kwa undani habari zinazohusu udhalilishaji sambamba na kuwataka kuwa na moyo wa kujitolea ili lengo la mafunzo hayoliweze kufikiwa.
Nae mkufunzi Ali Mbarouk Omar akiwasilisha mada ya Uandishi wa habari za uchunguzi amewataka waandishi hao kujenga uthubutu wakati wanapotekeleza majukumu yao kwa kuandika habari zenye ushahidi na kusoma nyaraka mbali mbali ili kuandika habari zenye kuleta tija na mabadiliko kwa jamii.
Jumla ya waandishi 15 kisiwani pemba wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuripoti habari zinazohisu udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto.