DC Mjaja: Wazazi, walezi wazuie watoto kuokota karafuu kuwakinga na udhalilishaji
15 August 2023, 4:38 pm
Mkuu wa wilaya ya Mkoani anawataka wazazi na walezi wasiwaruhusu watoto wao kuokota karafuu(mpeta) kwa kuhofia vitendo vya udhalilisha kwai matendo hayo yanaendezeka sana wakati wa msimu wa zao hili linapokuja kila mwaka.
Na Amina Masoud
Wazazi na walezi kisiwani Pemba wametakiwa kutokuwaachia watoto wao kwenda kuokota mpeta katika msimu wa zao la karafuu ili kuwalinda na vitendo vya udhalilisaji.
Akizungumza kwenye mkutano maalum uliowashirikisha kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya Mkoani na wanunuzi wa na wamiliki wa mashamba ya mikarafuu Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amesema katika kipindi hiki hujitokeza vitendo viovu vikiwemo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
Amesema tangu miaka ya nyuma zao hilo ni neema kwa wote ni vyema liendelezwe na lisiwe nakama kwa wengine.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha ununzi wa karafuu wilaya ya Mkoani Mohamme Iddi Hamad amewataka wananchi kuacha tabia ya kununua karafuu mbichi kwa kikombe sambamba na kununua kavu majumbani kwani inachangia kutokea kwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto na badala yake wafuate utaratibu uliowekwa na shirika hilo ili kuliongezea serikali pato la taifa.
Akifungua kikao hicho katibu tawala Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki amewaasa wanawake kutokuwaachia huru watoto wao kuokota mpeta na badala yake wawahimize kwenda kupata haki yao ya msingi ya elimu.
Wakichangia mada katika kikao hicho mwananchi Juma Kombo kutoka shehia ya mizingani na Neema Othman Haji wamesema vitendo vya udhalilishaji sio tu vinaathiri watoto hata wazazi wanaathirika hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja katika kupinga vita.
Kikoa hicho Kikao hicho cha siku moja kilicha washirikisha wamiliki wa mashamba wanunuzi wa karafuu mbchi na karafuu kavu kilichofanyika katika ukumbi wa umoja ni nguvu mkoani chenye lengo la kupiga marufuku ya ununuzi karafuu majumbani na kikiambatana na utembeleaji wa makabi ya mikarafuu katika maneno ya Mahudusi na Kwachangawe Mkoani.