Mkoani FM

WANAWAKE WASHIRIKI KWENE NGAZI ZA MAAMUZI , KISWAHILI CHAAJWA.

17 March 2023, 2:59 pm

NA KHADIJA RASHID, PEMBA.

“KISWAHILI kimenifanya niwe maarufu ndani na nje ya nchi yangu. Lugha hii niliipenda tangu nikizoma shule.

Licha ya umaarufu nilioupata kupitia Kiswahili, lugha hii imechangia maendeleo yangu binafsi na taifa kwa ujumla.”

Ni kauli ya Consalata Peter Mushi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), akizungumza na mwandishi wa makala hii katika mahojiano maalumu.

Mushi anasema, alianza kukipenda Kiswahili tangu alipokuwa Shule ya Msingi, mahaba yake katika lugha hiyo, yamemsaidia kukutana na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhudhuria dhifa na makongamano kadhaa ya kitaifa na kimataifa.

Anasema, miongoni mwa mafanikio binafsi kwenye orodha yake ya mafanikio, ni kuwa Katibu wa BAKITA.

Anasema, Lugha ya Kiswahili imekuwa kwa kiwango kikubwa na kwamba, si Tanzania pekee wanaozungumza lugha hiyo, hata nchi jirani wanazungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

Mmoja wa wajumbe wa Kiswahili katika kongamano hilo Diana Rose Oyuka kutoka Kenya, ni miongoni mwa mfano bora wa watu wanaozungumza Lugha ya Kiswahili vizuri. Kuttoka nchi yya Kenya.

Oyuka aliniambia pia ni mwalimu wa kufundisha lugha hiyo kwa wageni ambapo imempa umaarufu mkubwa hadi Tanzania.

“Mimi ni mwalimu wa Lugha ya Kiswahili katika shule maalum ya wasichana nchini Kenya, uwepo wangu hapa Zanzibar ni sehemu ya mafanikio yangu katika kupenda, kuzungumza na kufundisha Kiswahili nchini kwangu. Nimefika kwenye Kisiwa chenye marashi ya KARAFUU kwa sababu ya kuwa mdau wa Lugha ya Kiswahili kutoka Kenya,

Pia lugha hii imenifanya kua mjumbe wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU)” anasema Diana.

Kauthar Ishaq Mshtiti wa lugha ya Kiswahili kutokaPemba alisema, kuzungumza na kushriki kukuza Lugha ya Kiswahili, kulimpa fursa adhimu ya kuwa Mshehereshaji (MC) kwenye Kongamano la Kiswahili lililofanyika Washington, Marekani.

“Kupewa jina la MC Balozi Kauthar, kwangu ni kitu cha kujivunia sana, hata hivyo nimebadilisha hali ya uchumi wangu kupitia lugha yetu ya Kiswahili, jambo ambalo linanipa faraja zaidi,” amesema.

Saade Said Mbarouk, Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) anasema, Lugha ya Kiswahili ni sehemu muhimu katika maisha yake.

“Nilifundisha sana nikiwa mwalimu wa kawaida katika skuli tofauti za Unguja, lakini baada ya kumaliza Shahada ya Uzamili (Master), niliogolea kwenye bahari ya Kiswahili kwa kuchaguliwa kushika nafasi hii ya mwenyekiti”, anaeleza.

HARAKATI ZA KUANZA KUSAMBAZA KISWAHILI NJE YA NCHI

Katibu wa BAKIZA Consolata Mushi  aliweza kusambaza Kiswahili sanifu na fasaha ndani ya Tanzania na nje ya nchi hii akiamini ni fursa hasa kwa wanawake kwa vile wengi ni waalimu wa somo hilo kwa skuli za msingi na sekondari..

Akizungumza na Makala hii amesema hali hio imempa nguvu kama mwanamkee kiongozi.

Na kuongza kwa kusema kuwa Kiswahili kwake ni Faraja kwani ni chanzo cha kushika nafasi yya uongozi na kushiriki kahika harakai ofaui za kimaendeleo ya Kiswahili na kupata wigo na kuongeza ubunifu kwene uongozi wake.

“Nimefika mpaka nchini Uholanzi, Abudhabi na Burundi kwa kusambaza lugha ya kiswahili lakini pia nimeweza kubadisha maisha yangu binafsi kwa kiwango kikubwa Kiswahili kwani namudu maisha yangu na ndugu zangu kupitia lugha hii pia kimeniinua kiuchumi na kuniwezesha kuwa kiongozi” anasema Consalata..

Dr. Mwanahija,Ali Juma, Katibu Mtendaji BAKIZA kwake pia Kiswahili ni sawa na chakula cha siku kiasi ya kwamba, haiwezi kupita siku bila kukitumia kuongeza ubunifu na ufanisi wa kazi zake, lugha hio ndio chanzo cha kua Kaibu wa BAKIZA.

“Kiswahili kimesaidia kwa kiasi kibuwa kwani hata nafasi niliyonayo kwa sasa, ni kutokana na kuipenda , kuijua na kuifania kazi vizuri lungha ya Kiswahili,” amesema Dkt. Mwanahija.

“Vilevile Kiswahili kimenisaidia kujuana na watu wengi sambamba na kutembea mikoa tofauti nchini Tanzania na nchi kadhaa ikiwemo Afrika Kusini, hali iliyoniongezea umahiri katika kazi zangu na kunifanya kuwa mdau mkubwa katika kueneza Kiswahili, Katika hili najivunia sana.” Amesema Dkt.Mwanahija.

NCHI ZILIZOFANIKIWA KUPITIA KISWAHILI

Ukiacha Tanzania ambapo Lugha ya Kiswahili ndio lugha rasmi na lugha mama, zipo nchi ambazo zimefanikiwa kupiga hatua katika maendeleo kwa lugha hiyo.

Miongoni mwayo ni Kenya ambapo lugha kuu ni Kingereza. Lugha ya Kiswahili nchinio humo, iliwa ikizudiwa na ile ya Kingereza lakini sasa Kiswahili ni lugha rasmi nchini humo.

Kenya kwa sasa kuna skuli maalum ya kufundisha lugha hiyo, hali inayosaidia katika kukua kwa uchumi wa nchi hiyo na wanawake kushiriki kwene ngazi za maamuzi

 kwani wanawake wanaanza kujiajiri. Mfano nzuri ni Diana Rose Oyuka ambaye anafundisha lugha hiyo kwa wageni wanaotoka Marekani, Sudan na Uswis.

Kutokana na kazi hiyo, imemfanya Diana kuwa maarufu zaidi na kushika nafasi ya Ujumbe kwenye Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) pia Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA).

Kiswahili nchini Kenya na Tanzania hutumika kama lugha rasmi, sanifu, ya yzawa na Lugha ya Taifa.

Katika nchi nyengine kadhaa za Afrika ya Mashariki, lugha hiyo inatambulika kama Sanifu, Rasmi na lugha ya Kimataifa.

Ni dhahiri kwamba, lugha ya Kiswahili inaendelea kupata umaarufu wa kufundishwa Afrika kote na Ughaibuni.

Nchini Marekani, Kiswahili hutumika kuleta maendeleo kutoka nchi za Ulaya, China na hata za Afrika Mashariki, kwani hufundishwa watoto wao lugha hiyo, ili kuwa wafanyabiashara na viongozi wa baadae lengo kuongeza kipato.

Niliyajua hayo baada ya kukaa na Dk, Mahiri Mwita kwa takribani dakika 10 ambaye ni mwalimu wa Kiswahili nchini Marekani.

Pia alinieleza kuwa, ni vyema Watanzania wakaamka na kuendeleza Kiswahili ili kujipatia maendeleo na kushiriki kwne demokrasia na uongozi na sio kusubri ili kujinasibu kwa kusema ‘lugha hii ni ya kwetu,’ wakati hawaoneshi kuitendea haki ya kuikuza.

“Watanzania walio wengi wakihaha huku na kule kujifunza lugha za kigeni wakiamini ndio zinaweza kuwatoa kimaisha, na kushiriki kwene ngazi za maamuzi lakini kwetu Marekani tunaipigania lugha ya Kiswahili kama ni chachu ya maendeleo, na wapo wanashika nafasi za kuongoza kama vile kampuni kupiia lugha hii,” amesema Dkt. Mahiri.

Mwalimu Kato Herbert kutoka Kampala, Uganda anaefundisha katika skuli ya wanawake anasema, wanafunzi wake hawajawahi kuwa wa mwisho katika lugha hiyo.

“Nafundisha lugha ya Kiswahili katika skuli ya wanawake nchini Uganda, ila wanakua na mori wa kujifunza hali inayoniongeza ari ya mimi mwalimu, kwani wanajuhudi za vitendo zaidi, na wanaamini hio ndio fursa kwao za kufikia ndoo zao za kushiriki kwene uoaji wa maamuz” amesema Kato.

Mwamwingila Goima Mwamwingila, mtunzi na mwandishi wa vitabu kutoka Mtalimbo Books, anayasanifisha mawazo kupitia lugha hiyo, kwani hubadilisha udongo kuwa almasi.

“bBinafsi ni  shuhuda wa maendeleo ya wanawake kupitia luga ya Kiswahili, lakini pia tunajionea vitabu vingi vikiandikwa kwa lugha angavu na nyororo na hawa hawa wanawake, lugha ambazo zinakurejesha kuiona Zanzibar yenye mandhari ya kuvutia ndio kwanza watu wameshika silaha kumuondosha Mkoloni,” amesema Mwamwingila.

Walimu wataalamu wa Kiswahili katika Baraza la Kiswahili Tanzania ni 2,609 ambapo wanawake ni 1,478 huku Baraza la Kiswahili Zanzibar wakiwa 637, kati yao wanawake ni 453.

Mbali na kuwa lugha hiyo imekua dau kwa wanawake kuwa viongozi, kufundishwa na kuzungumzwa na watu kutoka mataifa mbalimbali,  hivi karibuni ilitambuliwa zaidi kimataifa na Shirika la Elimu ya Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Lugha ya Kiswahili imewekewa siku yake maalum ya kuadhimishwa duniani kote, ambayo ni Julai 7 ya kila mwaka, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa lugha hiyo.