Mkoani FM

ELIMU YA UJASIRIAMALI CHANZO WANAWAKE PEMBA KUSHIKA NGAZI ZA MAAMUZI.

17 March 2023, 2:32 pm

Na Amina Massoud Jabir

WANAWAKE wajasiriamali kisiwani Pemba wamewataka wanawake wenzao kutumia fursa zilizopo kwenye vikundi vya ujasiriamali kwani ni chanzo cha kushiriki kwenye harakati za demokrasia na uongozi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa kikundi cha KIHOGONI Hadia Ali Salim wakati akizungumza na mkoani fm na kuongeza kuwa ni wakati sasa kwa wanawake ni vyema kujiingiza katika harakati za kimaendeleo ikiwemo kujiunga kwenye vikundi na kugombania nafasi za uongozi kufanya hivyo kutasaidia kuwa viongzi bora hapo baadae.

Akitaja jambo lililomuhamasisha kuanzisha kikundi hicho amesema ni hali ngumu ya nmaisha hususan wanawake wanaoishi kijiji cha mauwani na kuokosa hamasa ya kujiendeleza na kushiriki kwenye maamuzi.

“nashukuru mara baada ya kuanzisha kikundi hiki  TAMWA kupitia mradi wa WEZA II wakaja kutupatia elimu ambayo inatusaidia hadi leo kwani mbali na elimu ya ujasiriamali pia walituwezesha kwenye uongozi na kwasasa tunajivunia hali iliyosaidia na taasisi ya  Milele Foundation nao kuvutika kuja kutupatia elimu ya ujasiriamali” amesema.

Rehema Ussi Juma Kufanya iasha na kupata maendeleo mazuri na kujikwamua na umasikini kwani wameweza kubadisha maisha yake.

Rehema ussi juma Amesema kupitia usimamizi wamwenyekiti Hadia ameweza kuondokana na utengemezi na kujuana na watu tofautijambo linalomuongezea uwajibikaji wa kiutendaji.

Nae Mwanaidi Juma Khamis amesema kwa sasa amekua kidume kwa vile utegemezi kwake umekuwa historia tangu kuanza kujiingiza katika kikundi hicho mwaka 2016.

Kikundi cha kihogoni kilichopo Mauwani shehia  ya kiwani kina jumla ya wanachama 16 wote ni wanawake wanaojishughulisha na utengenezaji sabuni, usarifu wa  mwani, mafuta ya mgando pamoja na kazi za mikono.