Mkoani FM

WANAZAWADIA: JUHUDI ZA KIONGOZI MWANAMKE AMINA ZAWAKOMBOA WANAWAKE.

17 March 2023, 2:41 pm

Na Amina Massoud Jabir.

WANAKIKUNDI cha ZAWADIA kilichpo changaweni Wilaya ya Mkoani wamepongeza jitihada zinazochukuliwa na kiongozi Amina Abdallah Said kwa kuwashaiwshi kuanzisha ushrika lengo kujikomboa na umasikini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katibu wa mwenyekit hicho Khadija Said Sultan amesema hapo awali hawakua na mwamko wa kufanya shughuli yoyote kujipatia kipato, ila ujio wa kiongo mwanamke huyo umemsidia binafsi kushika wadhifa alionao kwa sasa.

Amesema licha ya hali ya ulemavu alonayo bi Amina lakini ameweza kuanzisha kikundi ambacho kimewafungua macho wanawake wenye ulemavu na wasio na ulemavu na yeye ndio msimamii mkuu hali inayomjengea kujifunza Zaidi akiwa mwenyekiti kwani kitendo hicho kimekua ushawishi kwa wanwake wengine kujiingiza katika vikundi vya ushirika.

Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Nassra Yussuf  Khalfan amesema hakutarajia sikumoja kuona mtu mwenye ulemavu kuweza kuzalisha wazo ambalo litaikomboa jamii kupitia bi amina ameweza kuona kwamba kila mmoja anahaki na umuhimu wake katika jamii.

Mwankikundi Mwajuma Juma Mohammed na Tatu Ame Othman wamesema mbali na ulemavu wake lakini katika utendaji wake wa kazi bi Aminaanawashinda ambao hawana ulemavu.

Wameeleza kuwa kiongozi huyo ni wa kupigiwa mfano kwani anafanya kazi kama watu ambao wanavioungo kamili.

Kwa upande wake Amina Abdallah Said Muanzilishi wa kikundi cha SUBIRA NJEMA na kikundi cha ZAWADIA amesema amuamua kuchukua jukumu hilo lengo likiwa ni kuwewezesha wanwake na kuepukana na umasikini sambamba na kushiriki katikangazi za maamuzi.

Kikundi cha ZAWADIA kilianzishwa mwaka 2021 kikiwa na wanacha 13 chini ya muanzilisha Amina Abdallah Said.