Mkoani FM

WANAMAKANGALE WAMPONGEZA DC KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI.

17 March 2023, 2:09 pm

Na Khadija Rashid Nassor

Upatikanaji wa maji safi na salama shehiya ya Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ni miongoni mwa juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Mnamo mwezi wa 9 mwaka 2022 Changamoto hiyo imeripotiwa na Mkoani fm ikiwa Mkuu huyo wa Wilaya alichukua ahadi ya kulishughulikia tatizo hilo na sasa mafanikio yameanza kupatikana.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wanajamii kutoka kijiji cha Mawe Matatu na Mnarani Salma Omar na Time Ali   wamesema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano kwani kwa sasa pesa waliokua wanatumia  kununua maji inatumika kwa matumizi mengine ya kujiletea maendeleo ndani ya familia zao.

“tulikua tunatumia pesa nyingi kununua maji na wala hayaku ni toshelezi hasa nyumba zenye watoto ila kwa Mkuu wa Wilaya Bi Mgeni kutuletea hii huduma imeturahisishia na tunampongeza kwa kweli kwani anatekeleza majukumu yake kivitendo”

Kwa upande wake mfanya biashara ya uuzaji  maji Mohammed Sabri amesema kutokana na harakati za Mkuu huyo wa Wilaya ya Micheweni kuchngia na kusukuma  maendeleo binafsi suala hilo limemgusa na kuona ipo haja ya kutoa mashirikiano ili kuchochea maendeleo.

Sheha wa Shehiya ya Makangale Said Ali Kombo akizungumza kwa Shauku na Mkoani fm amesema juhudi za kiongozi Mgeni Khatib Yahya  ni za kupigiwa mfano  kwani anatekeleza kwa vitendo na kutatua changamoto zilizomo katika Wilaya yake lengo ni kufanikisha  maendeleo ya wananchi.

Suleiman Anass Afisa Uhusiano kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar Afisi ya Pemba amewaasa wanajamii   kutumia maji kwa uangalifu kwani kila tone ni gharama.

Akitoa ufafanuzi Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema hatua hiyo imefanikiwa kwa mashirikino ya pamoja kati yake na viongozi wa shehia, Jumiya ya Kwanini Foundation  pamoja na mfanya biashara ya kuuza maji ambapo kwa pamoja wameweza kutatua changamoto hiyo ya maji.

Jumla ya wakaazi 2,190 wa shehiya ya Makangale kwa sasa wamekua na uhakika wa upatikanaji wa huduma ya maji hali inayoashiri kupiga hatua kimaendeleo.