Mkoani FM

Wahamasishaji Jamii pemba watakiwa kuitunza miradi

21 September 2022, 12:25 pm

Dina Makota, Mratibu wa Mradi wa SWIL Kutoka Pengao

PEMBA.
Wahamasishaji jamii kisiwani Pemba wametakiwa kuongeza juhudi za kutoa uwelewa kwa jamii ili kuienzi na kuitunza miradi wanayoanzishiwa kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu kwa vizazi na vizazi.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa mradi wa swil kutoka taasisi ya PEGAO Dina Makota katika kiakao cha uwasilishwaji wa ripoti kutoka kwa wahamasishaji hao huko katika ukumbi wa maktaba chakechake pemba.Amesema,mbali na juhudi zinazochukuliwa na serikali , wahisani sambamba na taasisi mbalimbali ila jamii nayo inapaswa kuwa na tabia ya kutunza vile wanavyopatiwa ili viweze kudumu na kunufaisha kama lengo lilivyotarajiwa.

Wahamasishaji Jamii Kutoka  Pemba

Wakiwasilisha ripoti kwa niaba ya wenzao Safia Saleh muhamasishaji kutoka wilaya ya chakechake na maryam yussuf wilaya ya micheweni wamesema bado kuna changamoto nyingi katika jamii ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi na salama katika baadhi ya shehiya za chakechake sambamba na huduma duni za afya hali inayozorotesha maendeleo ya wanawake.

Kassim Nassor muhamashishaji wilaya ya mkoani na Sada Saleh Wilaya ya wete wamesema umbali wa skuli sambamba na elimu duni ya uongozi kwa wanawake nazo ni changamoto zinayopelekea kuwa kidogo katika ngazi za maamuzi.

Mbali na changamoto hizo wahamashishaji hao wameeleza yapo mafanikio ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwa watoto, mwamko kwa wanawake kushiriki katika ngazi za maamuzi na na kupata wahisani wanaosaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika shehiya ya Tibirinzi Chakechake jambo litakalopelekea waakazi wake na shehiya jirani kuondokana na shida hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.

Kikao hicho cha kujadili ripoti ni muendelezo wa vikao vya ufuatiliaji wa changamoto za jamii katika kuhakikisha wanawake wanashiriki katika ngazi za maamuzi na kufikia usawa zinazofanywa kupitia mradi wa SWIL na kutekelezwa na taasisi taasisi ya pegao, tamwa na zafela chini ya ufadhili wa ubalozi wa Norway nchini Tanzania.