TAMWA Zanzibar: waandishi wa habari wanolewa kuwasaidia wanawake kuwa viongozi
10 September 2022, 10:46 am
Uwepo wa asilimia ndogo ya ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi ni changamoto moja wapo inayopelekea kutopatikana kwa maendeleo kwa baadhi ya taasisi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania – Zanzibar Dr Mzuri Issa wakati akifungua mafunzo ya siku 5 ya kuwajengea uwezo waandiahi wa habari vijana huko katika ukumbi wa afisi hiyo tunguu wilaya ya Kusini Unguja.
Amesema bado hali ya ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi hauridhishi jambo lililochangiwa mitazamo potofu kwa baadhi ya wanajamii, hivyo ni vyema kwa waandishi wa habari wawe na muono wa mbali katika kusaidia jamii lengo kua na akiba mzuri itakayoleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa jamii na taifa kiujumla.
Dr. Ananilea Nkya mkufunzi katika mafunzo hayo amesema kiongozi anaeweza kujitolea ni rasilimali muhimu hivyo ni muda sasa kwa waandiahi kujitoa kuandika habari zitakazoonesha mwanga na kuongeza hamasa kwa wanawake kushinda wakati wanapojitolea kugombania nafasi mbalimbali.
Ahmed Iddi Haji na Amina Omar wamesema matarajio ya mafunzo hayo ni kwenda kuengeza uwelewa kwa wanawake kushiriki katika ngazi za maamuzi sambaba na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kuleta ufanisi wa kimaendeleo na kufanikisha lengo lamafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku tano yenye lengo la kuwajengea uwezo kuandika na kuchambua habari zinazohusu wanawake na uongozi kwa waandishi wa habari vijana 18 kutoka vyomba mbali mbali vya habari Zanzibar yaliyoandaliwa na Tamwa Zanzibar kwa Ufadhili wa National Endowment for Democracy kutoka Marekani yamefanyika katika ukumbi wa Tamwa Zanzibar Tunguu.