Kesi 39 za udhalilishaji zaibuliwa ndani ya robo mwaka Wete – Mkoani
22 August 2022, 4:52 pm
JUMLA ya kesi 39 za udhalilishaji wa kijinsiazimeibuliwana wanamtandaowa kupinga udhalilishaji ndani ya wilaya mbili kisiwani pemba.
Wakizungumza katika kikao cha kuwasilisharipoti hizo wanamtandao wa kupinga udhalilishaji wilaya ya wete na wilaya ya mkoani wamesema juhudi za pamoja kati ya wanajamii zimeweza kufanikisha kuibua kesi za matendo hayo.
Akiwasilisharipoti ya robo mwaka mwanamtandao kutoka Wilaya ya Mkoani Shabani Juma Kasim amesema katika wilaya hiyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu wameibua Jumla ya kesi 10 ikiwemo shehia ya Kangani, Mjimbini,Muambe, Mkoani mjini, Mtangani,Jombwe, Mtangani, Kirimdomo, Mjimbini,kiwani na Chambani.
Amesema miongoni Mwa kesi hizo zilizoripotiwa ni pamoja na kesi 8 za ubakaji,ambapo kati ya kesi hizo saba watuhumiwa wamekimbia na moja ipo mahakamani inaendelea kusikilizwa, kesi moja ya shambulio la aibu na kesi moja ya utelekezaji.
Kwa upande wake mwana mtandao kutoka Wilaya ya Wete,Siti Faki Ali amesema, wamefanikiwa kuibua jumla ya kesi 29 za matukio ya udhalilishaji, na kufanikiwa kuripoti kesi kumi na tatu 13 katika kipindi cha mwezi June hadi August zikiwemo kesi za kubaka saba 7, kesi ya kutorosha moja 1,kesi za kunajisi 1, udhalilishaji wa kingono moja 1 Na kesi ya kumpa mimba mwari 2.
Akiwasilisha ripoti iliyofanywa na wanahabari wachanga kwa wilaya 11 za unguja na ya mwaka 2022 iliyolenga kuangalia sababu zinazopelekea vijana na watoto wakiume kujiiingiza nkatika vitendo vya udhalilishaji Mratibu wa TAMWA Pemba Fat hia Mussa Said amesema jumla ya kesi 788 katika Wilaya hizo ikijumisha matukio ya ubakaji 692, kulawiti 100 na kunajisi 96 Na waathirika zaidi ni watoto walio chini ya umri wa miaka 18.
Afisa dawati la jinsia Wilaya ya Mkoani Rehema Mjawir Omar amesema bado jamii haijawa na utayari katika kuhakikisha wanashirikiana na vyombo husika kuwatia hatiani watuhumiwa jambo ambalo linarejesha nyuma juhudi hizo.
Mradi wa kumaliza vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, unaotekelezwa na chama cha waandishi wa habari Tanzania ‘Tamwa, Zanzibar, ambao unafadhiliwa na Shirika la kimataifa la maendeleo la Denmark (DANIDA) kupitia ubalozi wa Denmark Nchini.