Mbunge viti maalumu Pemba aomba watu wenye ulemavu wahesabiwe
21 August 2022, 2:43 pm
.
Wananchi Kisiwani Pemba wametakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa zoenzi la sensa litakapoanza siku ya tarehe 23/08/2022 kwani nao wana haki kama binaadamu wengine.
Kauli hiyo imetolewa na Mh Marya Azani mwinyi Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Kusini Pemba akitoa maelezo Mafupi kwenye bonza maalumu lenye lengo la kuihamasisha jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika sensa sambamba kuunga mkono zoezi hilo litakalofanyika hivi karibuni nchini Tanzania.
Amesem kuna baadhi ya wazazi na waelezi wanakuwa na tabia ya kuwaficha watoto wenyeulemavu hasa walemavu wa akili wakati wanapopita makarani wa sensa ili wasihesabiwe na kufanya hivyo ni kuwakosesha kupata haki zao za msingi kutoka serikalini.
Mkuu wa wilaya ya Mkaoni Khatibu Juma Mjaja ambae ni Mgeni Rasmi kwenye bonanza hilo amesema wakati wa sensa umefika sasa kila mwanachi awe tayari kuhesabiwa na kutoa ushirkiano wa utoaji taarifa sahihi wakati watakapopita makarani wa sensa kwani taarifa hizo ndio zitakazofanya serikali kuu kujuwa namna gani inapanga mahijati ya wanachi wake kulingana na sehemu husika .
Nicholaus Samson chibwana,katibu wa ccm wilaya ya Mkoani asema ameungana na viongozi wengini kuonesha na wao chama cha mapinduzi wilaya ya Mkoani wanaunga mkono katika zoezi zima la sensa ya watu na makaazi na kuwaomba wanachamo wote watoe ushirikiano wakati makarani watakapopita. Kwenye zoezi hilo.
Bonanza hilo limeandaliwa na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Kusini Pemba na kushirikisha vikundi mbali mbali vya mazoezi vinavyopatikana mkoani humo pamoja na timu mbili za basketball na timu ya rede kwa wanawake lenye lengo la kuunga mkono zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022 nchini Tanzania.