IUCN kupitia ubalozi wa Ireland Tanzania yang’arisha vikundi vya wajasiliamali Pemba
20 August 2022, 10:44 am
Wanavikundi cha Uvumbuzi Pujini Kibaridi,Mapape Cooperative Chambani na Yataka Moyo Chokocho wamelishukuru Shirika la IUCN kupitia mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland Tanzania kwa kuwasadia kwa hali na mali katika kuboresha vikundi vyao.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa ripoti fupi mara baada ya kufikiwa na ugeni wa Mkuu wa Mkoa uliombatana na wadau kutoka IUCN Fatma Haji Zarali kutoka ushirika wa Uvumbuzi wanaojishuhulisha na uzalishaji wa Chumvi, ukulima wa mboga mboga na uhifadhi wa mikoko amesema mradi huo umeweza kuwakomboa kwa kiasi kikubwa kwani kwa sasa miundombinu yao ipo imara,elimu ya uzalishaji bora na salama kwa mtumiaji,soko la uhakika hali iliyochangia kuongeza uzalishaji kutoka tani 4 hadi kufikia tani 20 kwa mwaka.
Kwa upande wa Mapape Cooperative wamesema kikundi chao kinajishuhulisha na ufugaji wa majongoo bahari, kaa,nyuki na uhifadhi wa mikoko ambapo kwa sasa wana jumla ya majongoo bahari 2700,zaidi ya kaa 250,na banda la kufugia nyuki lenye uwezo wa kuchukua mizinga 60 sambamba na kupeleka chuo cha bandari majongoo 20 kwa lengo la kufanyia utafiti na wakutotolesha vifaranga ili kufaidika na ufugaji huo.
Ameongeza pia kupitia mradi huo kumepatikana ajira 40 kwa jamii iliyowazunguka iliyojumuisha vijana wazee wa kike na kiume hali inayounga mkoano juhudi za serikali katika kukuza uchumi wa buluu na ajira kwa vijana na wazee.
Nao wanakikundi cha Yataka Moyo Chokocho wameushukuru Ubalozi wa Ireland Tanzania kupitia shirika la IUCN kwa ufadhili wa kuanzisha shamba mseto wa kilimo cha mwani na ufugaji wa majongoo na kupata mafunzo yaliosaidia kuongeza uzalishaji ukilinganisha na mavuno ya awali .
Akitaja lengo la Program ya ustahamilivu wa pwanani na bahari pia ni Mwakilishi kutoka IUCN Dr, Elinas Monga amesema ni kusaidia kukuza uchumi wa buluu kupitia uhifadhi shirikishi wa mifumo mikuu ya ikolojia na baionuai hali itakayosaidia utekelezaji mzuri wa sera ya uchumi wa buluu.
Dr, Monga ameeleza Program yao kwa sasa inafanya kazi na vikundi vinne viwili Pemba na viwili kutoka Tanga na kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kila kikundi kimepatiwa Tsh 29,000,000. Ikiwa ni ruzukuwa kwa utekelezaji wa mpango biashara ambao utaboresha na kukuza biashara zao
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja amewaeleza wanuafaika wa mradio huo kutumia vizuri fursa walizozipata na kuwa wabunifu wa shunguli nyengine zilizopo kwenye sekta ya uchumu wa bluu sambaba na kuendelea na shughuli zao hata baada ya kumalizika kwa mradio.
IUCN ni shirika la kimataifa linalojiusisha na uhifadhi wa maeneo asili ni shirika la wanachama na kwa sasa lina jumla ya washirika wanachama 1400 Duniani kote na linatekeleza program mablimbali ikiwemo Mabadiliko ya Tabianchi,Uhifadhi wa rasilimali maji,Masuala ya jinsia katika uhifadhi wa mifumo ya ardhi na ustahamilivu wa pwani na bahari, kwa sasa Pemba inatekeleza program ya ustahamilivu wa uhifadhi wa bahari iliyoanza mwezi wa tisa mwaka 2021 kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland Tanzania.