Mwenyekiti wa kamati ya abaraza la wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongoziwakuu ataka sharia ya mazingira ifutwe
12 August 2022, 11:38 am
ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa Mhe Machano Othman Said amewataka watendaji wa mazingira kuhakikisha kuwa sheria za mazingira zinafuatwa katika kuwalinda wanavikundi wanaojihusisha na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kikundi kinachojishughulisha na kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na utunzaji wa mazingira huko Chaani Kikobweni (HIMAKI ) amesema ,kuwepo kwa sheria hizo kutawasaidia wanavikundi kufanya kazi zao za kutunza mazingira kwa ufanisi .
Aidha Mwenyekiti huyo ameiomba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kushirikiana na Wizara ya kilimo Umwagiliaji Mali asli na Mifugo kuwaelimisha wakulima kupanda miti inayofaa katika maeneo yaliyopo karibu na vyanzo vya maji ili kuzuia vyanzo hivyo visiathirike na kukauka.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amesema Wizara yake imejipanga kupanda miti katika wilaya zote za Unguja na Pemba, kuviimairisha vitalu vya awali ili kuweza kuhifadhi mazingira na kuepuka athari za na mmong’onyoko wa ardhi nchini.
Waziri huyo amekipongeza kikundi hicho kwa juhudi wanazochukua za kulinda mazingira na kuwataka wasivunjike moyo na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ili kuleta manufaa kwa vizazi vijavyo.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa huo Makame Machano Haji amesema atahakikisha wanasimamia vyema kwa kuwapatia elimu na kuwaunga mkono katika masuala ya utunzaji wa mazingira.
Kamati hiyo imetembelea kikundi cha HIMAKI na mradi wa majiko nafuu katika Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja.