Mkoani FM

Wakulima wilaya ya Mkoani waomba wafikiwe na maafisa wa utabiri wa hali ya hewa

26 July 2022, 2:01 pm

 

WAKULIMA WA MPUNGA WA BONDE LA KIMBUNI PEMBA WAKIZUNGUMZA NA MKOANI FM

Wakulima wa kilimo cha mpunga bonde la kimbuni shehiya ya mgagadu wilaya ya mkoani kisiwani pemba wameiomba Radio Jamii Mkoani kuendeleza mashirikiano na wataalamu wa masuala ya kilimo kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuongeza ujuzi katika masuala ya kilimo.

Wakulima hao wakizungumza  na Mkoani fm ndugu,Abdalla Juma na Wahida khalfani wamesema tangu kuanza shughuli za kilimo hawakuwa na uelewa wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinasaidia katika kuongeza kipato cha mkulima.

Wameeleza tangu kujishughulisha na kilimo hicho hawajawahi kumuona mtaalamu vyoyote   kuwaelekeza kipindi gani walime  kilimo fulani  bali wanalima kutokana  namazoea walioachiwa na wazazi wao.

BONDE LA MPUNGA KIMBUNI WILAYA YA MKOANI PEMBA

 

Mkoani fm  imezungumza na Mkuu wa kitengo cha hali ya hewa kwa upande wa kilimo Ndugu Suleiman Ali Juma kutoka kituo cha utafiti wa kilimo matangatuani amesema, utabiri husaidia kwa kiwamgo kikubwa katika kuongeza uzalishaji kwani kufuatia utabiri mkulima anaweza kujua muda sahihi wa kutayarisha mashamba ili kuanza shughuli za kilimo.

Mpunga ni zao la pili la chakula linalolimwa nchini Tanzania, umuhimu wa zao hili umeongezeka kutoka muongo uliopita  na hii imekuja kutokana na jamii za mjini kupendelea zaid kula wali na kupunguza ulaji wa vyakula vyengine, na kulifanya zao hili kuwa la chakula na biashara.