Mkoani FM

UKOSEFU WA  HUDUMA ZA KIJAMII KIKWAZO KWA WANAWAKE KUWA VIONGOZI.

25 July 2022, 9:31 am

 

Ukosefu wa Huduma muhimu za Kijamii ni changamoto inayorejesha nyuma wanawake kufikia fursa katika demokrasia na  kujihusisha na harakai za uongozi.

Ameyasema hayo Mratibu wa Chama Cha Waandishi Wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) afisi ya ya  Pemba Fathiya Mussa Saidi wakati wa kufunga mafunzo ya siku Tatu kwa waandishi wa habari katika kuandika habari za wanawake na uongozi .

Amesema ,Ni wajibu kwa waandishi kuyatumia mafunzo waliyopatiwa kwa kufanya vipindi na kuandika habari zitakazoondoa changamoto hizo ili iwe ni  chachu ya  wanawake  kudai haki zao za kidemokrasia Na  kuleta maendeleo katika jamii.

Akifafanua dhima kuu ya mafunzo  mkufunzi Ali Mbarouk Omar amesema  ni  kuwasaidia waandishi wa habari  kuandaa maudhui ya  kihabri yatakayochochea maendeleo na wanawake kushiriki katika demokrasia siasa na uongozi.

Habiba Zarali Rukuni kutoka gazeti la Zanzibar Leo Na Salum Msellem kutoka Radio Istiqama wameishukuru tamwa kwa kuendelea kuwajengea uwezo wa namna ya kuandika habari zenye ubora wa kuibuwa vikwazo vinavinyima haki ya wanawake na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo ili lengo la mradi huo liweze kufikiwa.

Mafunzo haya ni muendelezo wa kuwajengea wanawake kushiriki kwenye ngazi  za maamuzi yametolewa na TAMWA ZANZIBAR kwa kushirikiana na ZAFELA Na PEGAO kwa efadhili wa ubalozi wa Norway nchini Tanzania.