Wananchi Kisiwa Panza walia na Maji safi na salama.
23 October 2021, 1:08 pm
Na Said Omar Said
Wakizungumza katika mkutano wa kueleza changamoto zao mbele ya mkuu wa Wilaya ya Mkoani katika kisiwa hicho wamesema suala la maji limekuwa changamoto kiupande wao kutokana na maji kutokufika katika makaazi yao.
Wamesema kutokana na umuhimu wa huduma ya maji hulazimika kukesha bila ya mafanikio na badala yake hulazimika kununua maji ambapo dumu moja shilingi 500 au hupaswa kutembea wastani wa kilimita 3 kuiifuata huduma hiyo katika kijiji cha Mtondooni.
Wakizungumzia suala la elimu wananchi hao wameonesha wasiwasi wao juu ya usalama wa watoto wao kutokana na ubovu wa daraja linaounganisha kijiji cha panza na mtondooni ambacho ndiocho chenye skuli.
Aidha wameelezea changamoto ya kukosekana sehemu ya huduma ya uzazi katika kituo cha afya jambo ambalo linawatia hofu akina mama wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja akitoa ufafanuzi juu ya changamoto mbali mbali amesema serekali imeshatenga bilioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa huduma mbali mbali za kijamii kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amemuagiza Afisa wa Maji wilaya Mkoani kuongeza siku za utoaji wa huduma hiyo katika kisiwa hicho kua siku 3 badala ya 2 kwa wiki.
Sambamba na hayo ametumia fursa hio kuwataka wananchi hao kuiyunga mkono serekali ya Mapinduzi Zanzibar katika mapambano dhidi ya Udhalilishaji wa kijinsia na kuwafichua wanaofanya matendo hayo.
Nae Mkurugenzi baraza la Mji Mkoani Yussuf Kaiza Makame amewataka wananchi hao kuyatumia mifuko ya jimbo kwa kuandika barua ili aweze kutatuliwa changamoto zao.
Akijibu changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji Afisa wa Maji wilaya ya Mkoni Mkubwa Mnyaa Mbarawa amekiri kuwepo kwa changamoto hio na amesema tayari wameshafikiria kujenga tangi kubwa la maji kwa ajili ya watu wa kisiwa panza.
Akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa huduma ya uzazi katika kituo cha afya Kisiwa Panza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni, Moh’d Faki Saleh amesema serekali imejipanga katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 kuvipandisha hadhi vituo vya afya kutoka daraja la kwanza hadi la pili pamoja na kuweka sehemu ya kujifungua, kituo cha afya kisiwa panza kikiwa miongoni mwao.
Mkutano huo na wananchi uliowajumuisha maafisa mbali mbali wa serekali ya wilaya ya Mkoani ni muendelezo wa ziara zake katika kuskiliza changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.