Highlands FM
Highlands FM
24 June 2025, 12:09

Takwimu za jeshi la polisi zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2023, matukio ya ajali za barabarani yalikuwa 1,733 katika kipindi cha Januari hadi Desemba, na kusababisha vifo 1,118.
Na Samwel Mpogole
Jamii imetakiwa kufuata na kuheshimu sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali, ghasia na changamoto nyingine zinazotokana na uvunjifu wa sheria hizo.
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto kutokufuata sheria za barabarani jambo linalopelekea usumbufu na wakati mmwingine kusababisha ajali,
Katika kukabiliana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Bw. Furaha Malele, anatoa wito kwa wananchi kufuata sheria, taratibu na alama za barabarani ili kulinda maisha yao na ya wengine.
Kwa upande wake, Said Mohamed Madudu, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini – LATRA CCC Mkoa wa Mbeya, amewakumbusha abiria kutambua haki zao, ikiwemo kudai tiketi wanapopanda vyombo vya usafiri wa umma.
Viongozi hao wamehimiza ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya dola, ili kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa maslahi mapana ya taifa.