Highlands FM
Highlands FM
26 May 2025, 12:43

Dkt Juma Homera. Picha na Samwel Mpogole
Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kushiriki maonesho ili waweze kunufaika na fursa lukuki.
Na Samwel Mpogole.
Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Mbeya imeandaa maonesho makubwa ya kibiashara yaliyoanza Mei 23, mwaka huu, katika viwanja vya Soko la Uhindini, yakilenga kuwawezesha wananchi kupata elimu na kutambua fursa mbalimbali za biashara, viwanda na kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho hayo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi.
Dkt. Homera amesema biashara ni kichocheo cha mahusiano mazuri baina ya nchi na nchi, hivyo amewataka wadau wa sekta binafsi, hususan wamiliki wa hoteli, kutumia fursa hii kujitangaza na kuongeza kipato.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti Biashara TCCIA Mkoa wa Mbeya, Bw. Muhsin Mkongo, ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia maonesho hayo, huku akibainisha utofauti mkubwa wa mwaka huu ukilinganisha na miaka iliyopita.
Sauti ya Muhsin Mkongo – Makamu Mwenyekiti wa Biashara, TCCIA Mbeya