Highlands FM
Highlands FM
22 May 2025, 13:33

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wanawake wawili, Seva Simwinga (29) na Sara Simwinga (35), wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Mponja, Uyole jijini Mbeya, kwa tuhuma za kupatikana na shehena ya dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 320.
Na Samweli Mpogole
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, (SACP) Benjamini Kuzaga, amesema watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa Mei 21, 2025, katika oparesheni maalum iliyofanywa na jeshi hilo katika Mtaa wa Mponja, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, jijini Mbeya.
Katika tukio jingine, Kamanda Kuzaga amesema kuwa jeshi hilo pia linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na bhangi yenye uzito wa kilogramu 30.
Sambamba na hilo kamanda kuzaga ametoa wito kwa baadhi ya wananchi wanao jihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya kuacha mara moja kwa lengo la kulinda afya ya jamii na kujenga taifa imara lenye nguvu.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mtandao mzima wa usambazaji wa dawa hizo hatari katika maeneo mbalimbali ya nchi.
