Wananchi waipa heko tume ya ushundani {FCC} nyanda za juu kusini
9 July 2024, 17:17
Na Lameck Charles
Highlands Fm Mbeya
Wananchi wilayani kyela mkoani mbeya wameipongeza tume ya ushindani (FCC) Kanda ya nyanda za juu kusini kwa kuendelea kuwapa elimu kuhusu haki za mlaji na viashiria vya bidhaa bandia.
Wameyasema hayo kwenye maonesho ya biashara yafahamikayo kama Kyela Exbition yaliyofanyika kwenye viwanja wa kasumuu kyela.
Andason luiza ni Mkaguzi na ofisa toka tume ya ushindani amesema wananchi wameneshwa kushtushwa na uwapo wa bidhaa bandia mtaani huku wakishukuru tume hiyo kuwapa elimu itakayowasaidiam kufanya utambuzi wa bidhaa bandia.
Dicksn Mbanga ni mkuu wa kanda wa tume ya ushindani FCC nyanda za juu kusini amesema wametoa elimu kwenye viwanja hivyo vya kasumulu Kyela ukizingatia eneo hilo lipo mpakani mwa Tanzania na Malawi hivyo ni vyema wananchi wawe na uelewa kuhusu bidhaa bandia.