Highlands FM

Wananchi watakiwa kutoa malalamiko juu ya huduma za nishati na maji

30 May 2024, 17:13

Francis Mhina Afisa Huduma kwa wateja  (Ewura) nyanda za juu kusini

Na Lameck Charles

Wananchi wa nyanda za juu kusini wametakiwa kuendelea kutoa malalamiko yao wanayokabailiana nayo pale wanapopata huduma zinazohusishwa huduma za nishati na maji.

Kauli hiyo imetolewa na Francis Mhina Afisa Huduma kwa wateja  (Ewura) nyanda za juu kusini amesema EWURA itaendela kutoa elimu kwa wananchi kwani wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha ni wapi wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao.

Sauti Francis Mhina

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura ni moja ya taasisi iliyoshiriki kwenye maonesho ya Mbeya Expo 2024 yaliyofungwa hii leo katika viwanja vya City Market Square uhindini jijini Mbeya.

Mkuu wa wilaya ya mbeya Benno Malisa alipotembelea katika banda la Ewura katika maonesho ya Mbeya Expo 2024