Highlands FM

Wananchi chunya waomba kutatuliwa changamoto ya maji

30 May 2024, 16:37

Mwananchi wilaya ya chunya akiongea na mwandishi wetu kuhusu changamoto ya maji katika eneo hilo.

Na Pascal Ndambo

Wananchi  wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameiomba serikali kutatua changamoto ya maji ambayo wamedai kuwa imedumu kwa muda mrefu na kusababisha adha ya kufuata maji ya visima umbali mrefu ambayo sio safi na salama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema changamoto ya maji katika kata ya Itewe na baadhi ya maeneo wilaya ya Chunya imekuwa ni kubwa jambo ambalo limewasahaulisha ni lini wameyaona maji ya bomba yakitoka, hivyo wameiomba serikali iwatatulie changamoto hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amekiri uwepo wa changamoto ya maji hasa Chunya Mjini lakini amebainisha wilaya hiyo imetengewa bajeti ya Zaidi ya billioni 17 kwa ajili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safiu na salama

Taarifa kamili na Na Pascal Ndambo

Sauti Pascal Ndambo
Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka