Wakulima 200 Mbeya wapewa mafunzo ya mboga na matunda
29 November 2023, 17:56
Na Samwel Mpogole
Zaidi ya wafanyabiashara na wakulima 200 wa mboga na matunda katika mikoa ya Songwe na Mbeya wamefuzu mafunzo ya ulasama wa chakula ambapo yamelenga kuongeza mnyororo wa thamani kupitia shughuli za uzalishaji .
Mafunzo hayo yametolewa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Rikolto ambalo limeendelea kutoa mafunzo hayo katika mikoa ya mbeya na songwe.
Akifunga mafunzo hayo ,Mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera ambaye amewakilishwa na mkuu wa wilaya ya mbeya Benno Malisa amewataka wahitimu kutumia mafunzo kuongeza Thamani ya mazao ya mboga na matunda.
Mratibu wa shirika la Rikolto mkoa wa mbeya ,Shukuru tweve amesema ili kuhakikisha wakulima na wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga wanapata tija mafunzo na vifaa vi nyenzo muhimu kifikia lengo hilo.
Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara mkoa wa mbeya {TCCIA } Erick Sichinga ameeleza kuwa kuwapata washindi haikuwa kazi rahisi kwani vigezo na taratibu zilizozingatiwa kufika hapo walipo fika.