‘Feed the Future’ yatoa mafunzo kwa wakulima wa Mboga na Matunda Mbarali
15 November 2023, 14:58
Na Mawanaisha Makumbuli
Na Mwanaisha Makumbuli
Shirika lisilo la kiserikali feed the future wakishirikiana na USAD kutoka nchini marekani wamewapatia mafunzo wakulima wa mboga mboga na matunda namna bora ya kulima kilimo chenye tija katika mikoa ya Njombe, Morogoro ,Iringa na Mbeya.
Mkurugenzi wa mradi wa USAD kilimo tija ANTONIO COELLO amesema kuwa mradi huo umewafikia wakulima na vikundi mbalimbali namna ya kulima kilimo chenye tija ambapo baadhi yao waliweza kufanya vizuri kupitia mradi huo.
Naye mkuu wa wilaya ya mbarali Denisi mwila akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya amesema kuwa mradi wa kilimo tija umetoa mchango madhubuti katika kutekeleza muunganiko kati ya wadau mbalimbali huku mafanikio yakionekana kwa wakulima kupitia mradi huo.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima fanueli zakayo mahaye amemewataka wadau hao kuendelea kutoa mafunzo kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija na kuwatafutia masoko nje ya nchi licha ya changamoto wanazopitia kwa sasa juu ya kuuza mazao yao kwani yamekuwa yakiharibika kutokana na kukosa kwa soko.
Kilimo ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu ambayo humsaidia kupata mazao kwa ajili ya chakula na mazao mengine kwa ajili ya biashara ambayo inaweza kumuingizia kipato kwa ajili ya maisha yake, pia kipato hicho husaidia katika kukuza uchumi wa nchi yake.